MWANAMUZIKI nyota wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’
kesho (Jumatatu) anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni kufuatia
taarifa alizofikishiwa Meneja na mume wa msanii huyo, Gadna G Habash
‘Captain’.
Gadna alisema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa Lady Jaydee kufika Mahakama ya Kinondoni, kesho (Jumatatu) Mei 13, mwaka huu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni, hii ni baada ya kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo jana na kuleta barua ya kumkabidhi Lady Jaydee mwenyewe japo hawakumkuta” alisema Gadna.
Katika ukurasa wa Twitter wa Lady Jaydee saa tatu zilizopita aliandika hivi "Sumu ya teja Ukonga, Keko, Segerea. Kesho Mahakamani kizibiti ubaoniii eeeh aaah!" wakati siku ya Ijumaa katika ukurasa wake wa Facebook aliandika hivi:

"Ratiba
ya usiku wa leo ni MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu
natakiwa Mahakama ya Kinondoni... Taarifa zaidi zitafuata nikijua
kinachoendelea... Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk
asubuhi."
No comments:
Post a Comment