Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili
amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na
moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana
na sababu za kimaadili kwenye tiba,Muhimbili hospitali hawawezi kusema
rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo, Aminiel amesema Marehemu Langa
alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa
kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa
kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia
No comments:
Post a Comment