My Creation

Wednesday, 3 July 2013

Cpwaa sasa kujulikana duniani na ulimwenguni kote


Cpwaa amesaini mkataba na  moja ya lebo kubwa kabisa za muziki duniani “Universal Music, South Africa”.Maudhui yake yatasambazwa kupititia Kleek ( mobile streaming service) inayopatikana kwenye simu zote za Samsung (Smart phones) katika nchi za  Ghana, Angola, Kenya, South Africa na Nigeria.

 CPwaa ni mmoja kati ya wasanii namba moja waliosainiwa na Universal Music kutoka East Africa kwa ajili ya Kleek continental platform.

 March 13, 2013 Universal Music Group, wakishirikiana na Samsung pamoja na lebo za Africa na za kimataifa, wamezindua pan-African mobile music streaming service inayoitwa Kleek, iliyodizainiwa na kutengenezwa kwa ajili ya Africa .

 Kleek itawaweka karibu wapenzi wa muziki na wasanii wao wanaowapenda, huku ikiwapatia nafasi muhimu kwa wasanii kuwa na access na watu wengi 
Licha ya kupata mapato kupitia mziki wake, Cpwaa pia atapata nafasi ya kujulikana duniani na ulimwenguni kote kupitia Kleek.

No comments:

Post a Comment