Huyu ndio Iryn Namubiru, mwanamuziki kutoka nchini Uganda ambaye
ameripotiwa kukamwatwa huko nchini Japan kutokana na tuhuma za
kupatikana na dawa za kulevya.Ripoti zinaweka wazi kuwa, Iryn alienda nchini humo kwaajili ya
kufanya show Jumamosi iliyopita, Tarehe 4 huko Tokyo, Yotsukaido
Cultural Hall, na hadi dakika ya mwisho ya mpango huu, promota aliingia
mitini, issue iliyomlazimu Iryn kuripoti tukio hili polisi.Story kwa mtaa ni kwamba kabla ya ziara hii, Iryn alikuwa apae
kuelekea Japan sambamba na Dr Hilderman pamoja na King Michael lakini
hawa wengine walichomoa hasa baada ya promota huyu aliyetambulika kwa
jina la Kim Ueno kushindwa kuwalipa kiasi walichokubaliana kama advance
kwaajili ya show na kwaajili ya ticketi zao za ndege kurudi Uganda.
No comments:
Post a Comment